Job 23

Hotuba Ya Nane Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Kulalamika Kwangu Ni Uchungu

1Ndipo Ayubu akajibu:
2 a“Hata leo malalamiko yangu ni chungu;
mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua.

3 bLaiti ningefahamu mahali pa kumwona;
laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!

4 cNingeliweka shauri langu mbele zake,
na kukijaza kinywa changu na hoja.

5 Ningejua kwamba angenijibu nini,
na kuelewa lile ambalo angelisema.

6 dJe, angenipinga kwa nguvu nyingi?
La, asingenigandamiza.

7 eHapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake,
nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.


8 “Lakini nikienda mashariki, hayupo;
nikienda magharibi, simpati.

9 fAnapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni;
akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.

10 gLakini anaijua njia niiendeayo;
akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

11 hNyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu;
nimeishika njia yake bila kukengeuka.

12 iSijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake;
nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.


13 j“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga?
Yeye hufanya lolote atakalo.

14 kHutimiliza maagizo yake dhidi yangu,
na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba.

15 lHiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake;
nifikiriapo haya yote ninamwogopa.

16 m nMungu ameufanya moyo wangu kuzimia;
yeye Mwenyezi amenitia hofu.

17 oHata hivyo sijanyamazishwa na giza,
wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.

Copyright information for SwhKC